- Kiongozi wa chama cha ODM, Raila Odinga amemjibu vikali Moses Wetang'ula kwa kumhusisha na masaibu ambayo yamekuwa yakimkumba siku chache zimepita
- Wetangula alidai kuwa uhusiano wake na Raila uligonga mwamba na kwamba kiongozi huyo wa ODM ndiye aliyeshinikiza kuondolewa kwake katika wadhifa wa Kiongozi wa Wachache Seneti
Chama cha ODM, kinachoongozwa na Raila Odinga kimejitokeza kumrarua kiongozi wa chama cha Ford Kenya, Moses Wetang'ula kutokana na matamshi yake ya hivi punde dhidi ya Raila Odinga.
Habari Nyingine: Gavana Mutua amdhihirishia mkewe kuwa ndiye bora kuliko wote, amwonyesha makuu ya dunia
Katika taarifa iliyowasilishwa na msemaji wa Raila Odinga, Dennis Onyango, Wetangula amekuwa hivi majuzi akimhusisha Raila Odinga kwa masaibu yanayomkumba hasa kuondolewa katika wadhifa wake kwenye Seneti na kamwe hafai.
Tuma neno ‘NEWS’ kwa 40227 ili kupata habari muhimu pindi zinapochipuka
Habari Nyingine: Mfahamu mwanamume Mkenya anayetumia mamilioni ya pesa kujigeuza kuwa mwanamke
Kulingana na Onyango, Wetangula kwa kuendelea kumshambulia Raila kila mara kumedhihirisha kuwa ana tofauti za kibinafsi na kiongozi huyo wa ODM.
Habari Nyingine: Unamjua vyema mwakilishi wa kike wa Murang’a Sabina Chege?
" Juhudi zake Wetangula za kila wakati kutaka kukwepa ukweli na kumwelekezea Raila Odinga lawama kwa masaibu yake yadhihirisha ana tofauti za kibinafsi," Alisema Onyango kwenye taarifa iliyoonekana na TUKO.co.ke.
Matamshi ya Onyango yanajiri siku chache tu baada ya Wetang'ula kutangaza kujiondoa kwake katika muungano wa NASA na kutamatisha uhusiano wake wa kisiasa na Raila Odinga.
Read ENGLISH VERSION
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri: mwangi.muraguri@tuko.co.ke
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdibH15fo9mn5qml5a2rK2MqZyknV2urqy7jLCYnKCRYri2usihrKyho52ubrrAZqSaq5Ger7Z52JqiqGWilratrYyapLCZnZe2onnWnquappequaJ6x62kpQ%3D%3D