Wengine waliokuwa wakijivinjari na vileo walifanikiwa kuwatoroka polisi ambao walinasa kreti kadhaa za mvinyo jinsi K24 Digital iliripoti.
Miongoni mwa waliokamatwa ni mmiliki wa baa hiyo, ambaye kulingana na polisi amenaswa mara mbili akiendeleza baishara yake ya kuuza pombe usiku licha ya serikali kuagiza kufungwa kwa maeneo yote ya burudani.
Wenyeji kadhaa walielezea kuudhika kwao na jinsi baadhi ya wakazi wanakaidi maagizo ya serikali ya kusalia manyumbani nyakati za usiku, na kuwalazimu polisi kutumia nguvu zaidi katika kukabiliana nao.
Washukiwa walipelekwa kituo cha polisi cha Kayole wakisubiri kufikishwa mahakamani Kasarani.
Chanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdjaoZ4fJJmopqxn6GybsPAraxmbV2srqytzJqrsJldrK6stcSnnKWdqpZ6o7XArJ%2BaqpFixqJ5wZqYZq2jnri2esetpKU%3D